Paul Makonda: Vita dhidi ya ushoga Dar es Salaam si msimamo wa serikali

Paul Makonda

Chanzo cha picha, MAKONDA INSTAGRAM

Serikali ya Tanzania imejitenga na kampeni ya kuwakamata na kushtaki mashoga inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania iliyotolewa Jumapili, Novemba 4 inadai kampeni hiyo ni mawazo binafsi ya Makonda na si msimamo rasmi wa serikali.

"Serikali ya Tanzania ingependa kufafanua kwamba hayo ni mawazo yake (Makonda) na si msimamo wa Serikali."

Katika taarifa hiyo, serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa ambayo imeisaini na kuiridhia.

"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba," imesema taarifa hiyo.

Tarifa hiyo ya aina yake ni ya kwanza kutolewa na Tanzania kuhusiana na masuala ya ushoga, na inaonesha taifa hilo kwa kiasi fulani limelegeza kamba juu ya vitendo hivyo.

Katika miaka ya hivi karibuni serikali ya Tanzania imevifunga vituo kadhaa visivyo vya kiserikali kwa madai ya kuchochea ushoga kwa kutoa elimu ya mahusiano ya jinsia moja.

Tamko la serikali

Oktoba 31, Makonda aliongea mbele ya wanahabari na kusisitiza kuwa haki za wapenzi wa jinsia moja hazitambuliki kama haki za binaadamu Tanzania.

Katika mkutano huo, Makonda alitangaza vita yake mpya dhidi ya ushoga na kuunda kamati mahususi ya watu 15 kuongoza mapambano hayo.

Kwamujibu wa sheria za Tanzania, kufanya mapenzi 'kinyume na maumbile' ni kosa la jinai ambalo mtu akikutwa na hatia adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 au maisha jela.

Baada ya Makonda kutangaza vita yake, Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kuwa watalii wenye uhusiano wa jinsia moja hawataruhusiwa kuingia Tanzania.

Hata hivyo, Kigwangala baadae alifuta ujumbe huo bila kutoa taarifa yeyote.

Hata hivyo wapo ambao walishaanza kumkabili waziri huyo wakimtahadharisha kuwa kauli yake italeta athari kwenye soko la utalii ambalo limekuwa likichangia pakubwa katika uchumi wa Tanzania.

Kama ilivyo katika kampeni nyebgine ambazo Makonda amekuwa akizianzisha upinzani ulikuwa mkubwa kwake.

Ruka Twitter ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Raisi wa chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) Bi Fatma Karume akitumia mtandao wake wa Twitter alitangaza kuwatetea mashoga akisema kuwakamata ni kuwashitaki ni kinyume cha haki za binaadamu.

Ruka Twitter ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

Bi Karume pia amedai sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja ni kandamizi na inaenda kinyume na katiba.

Baada ya serikali kutangaza kujitenga na Makonda wapo wanaotaka aondolewe madarakani, lakini hilo linaweza lisiwe jambo rahisi.

Ruka Twitter ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Mwisho wa Twitter ujumbe, 3

Mapema mwaka huu Makonda aliingia katika mzozo na Waziri wa Fedha Dkt Philip Mpango na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya Makonda kutaka kuingiza makontena yanayodaiwa kuwa na samani za walimu bila kuyalipia kodi.

Samani hizo zinatoka Marekani ambapo Makonda anadai alichangiwa na Watanzania waishio huko. Makontena hayo yamekwama bandarini ambapo Makonda alikuwa anataka apewe msamaha wa kodi.

Mzozo huo ulihitimishwa na Rais John Pombe Magufuli mwezi Agosti kwa kumtaka Makonda alipe kodi anayotakiwa. Wengi walidhani huo ndio ungekuwa mwisho wa Makonda lakini haikuwa.